Awavutia watu kwa ustadi wake wa kupepeta mpira

Video fupi inayomuonesha mwanadada Hadhara Charles Mnjeja kutoka Tanzania, akipepeta mpira kwa ustadi imepata umaarufu mkubwa katika mitandao ya kijamii. Rais wa Marekani Donald Trump alitambua kazi ya Hadhara na kuandika katika mtandao wake wa Twitter kuwa ni kipaji kinastahili kukuzwa. Mchezaji huyo wa miaka 29 yuko nchini Malawi hadi mwezi Machi ambako anajipatia riziki kupitia onyesho lake mitaani. Analipisha dola tano kupepeta mpira kwa dakika mbili.Je anasemaje baada ya kutambuliwa na Trump? "Nashukuru kuwa rais Trump anajua jina langu. Hatahivyo namuomba anisaidie kukuza kipaji changu kiwe baishara imara."

Wed, 27 Feb 2019 03:56:18 GMT

Shabiki wa Yanga aliyemweka rehani mkewe

Je unaweza kumweka mkeo au mumeo rehani ukiwa na matumaini kuwa timu unayoishabikia itashinda mechi yake dhidi ya mpinzani wake wa jadi? Mwanamume mmoja ambaye ni shabiki sugu wa timu ya Soka ya Yanga nchini Tanzania alimuweka mkewe rehani kwa matumaini kuwa timu hiyo itaishinda Simba katika mechi ya ligi kuu, lakini kwa bahati mbaya ikapoteza mechi hiyo na sasa mkewe amekimbia nyumbani kwa hofu ya kutwaliwa na shabiki huyo wa Simba.

Wed, 20 Feb 2019 13:31:03 GMT