Manchester United yaanza harakati za kumtafuta mrithi wa Ole Gunnar Solskjaer: Nani atakayejza pengo lake?

23 Noviembre, 2021

Makocha wanaosakwa na United
BBC

Michael Carrick hakupatiwa kipindi cha muda fulani na naibu afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Manchester United Ed Woodward wakati alipotakiwa kujaza pengo lililowachwa wazi na kufutwa kwa Ole Gunnar Solskjaer. Inaonekana kana kwamba Carrick atasalia katika timu hiyo kuiongoza katika mechi dhidi ya Chelsea ugenini baada ya kusimamia mechi ya jumapili ya kombe la klabu bingwa dhidi ya Villareal.

Kuna siku nne kabla ya United kucheza dhidi ya Arsenal katika katika uwanja wa Old Trafford tarehe 2 Disemba na kufikia wakati huo kutakuwa na mwelekeo kwa wale wanaoona ni mkanganyiko katika klabu hiyo.

BBCSport inachanganua changamoto wanazokumbana nazo United ili kumuajiri mkufunzi anayeweza kuleta ufanisi katika klabu hiyo.''Kwa jumla tumeshindwa kutoa matokeo mazuri''.

Kwanini United inahitaji kaimu mkufunzi?

Katika taarifa wakithibitisha kuondoka kwa Solskjaer , United ilisema kwamba inataka kumchagua kaimu mkufunzi kumaliza msimu huu . Maneno hayo yalionesha kwamba mkufunzi wanayemtaka hatakuwepo hadi msimu wa joto ujao na kwamba hawaamini kwamba Carick ambaye hajawahi kuwa mkufunzi , ni chaguo mbadala kuchukua wadhfa huo kwa kipindi cha kampeni kilichosalia.

Licha ya kwamba mpango huo umezongwa na mikanganyiko , ina maana kwamba klabu hiyo itamuajiri mkufunzi mpya kwa misingi kwamba itaendelea kujimudu kwa muda wa miezi sita kabla ya kumpata mkufunzi huyo. Ni wakufunzi wazee wasiotaka kandarasi ya muda mrefu ambao wangejipata kuvutiwa na kazi hiyo kwasasa.

Steve Bruce ametajwa lakini, licha ya kuwa mchezaji wa zamani wa United, miezi yake ya mwisho kama mkufunzi wa Newcastle haiwezi kutoa motisha miongoni mwa mashabiki na United wana kipindi cha muda mrefu kubadili matokeo mabaya msimu huu.

Wengine wanafikiria kwamba sir Alex Ferguson , ambaye ana uzoefu mkubwa zaidi ya mtu yeyote katika mchezo huo, anaweza kutumika kujaza pengo la muda , lakini ukweli ni kwamba raia huyo wa Uskochi ana umri wa miaka 79 kwa sasa.

Majina yaliotajwa kurithi wadhfa huo - Beki wa zamani wa United Laurent Blanc na kocha Ralf Rangnick tayari wana kazi.

Blanc ni mkufunzi wa klabu ya Qatar ya Al Rayyan , ambapo msimu jutaendelea hadi Machi mwaka ujao. Rangnick ni mkurugenzi wa kiufundi katika klabu ya Lokomotiv Moscow, ambaye alikiri kwamba atachukua likizo katikakati ya mwezi Disemba.

Lucien Favre amekuwa nje tangu alipofutwa kazi na Borussia Dortmund 2020. Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 64 amehusishwa na ukufunzi wa klabu chungu nzima katika ligi ya premia na alikuwa aajiriwe kuwa mkufunzi wa Crystal Palace msimu uliopita kabla ya kukataa kazi hiyo.

Je ni nani anayefanya uamuzi?

Kufuatia kutibuka kwa mpango wa ligi ya Superleague Ulaya, naibu afisa mtendaji wa Man United Ed Woodward ataachia ngazi mwisho w mwaka huu.Wakati huohuo, wengi walihisi kwamba ni wakat wa kipindi chamajira ya joto kijacho.

Lakini Woodward anasalia katika wadhfa wake huku ikiwa haijulikani iwapo atakata mahusiano yake na United wakati atakapojiuzulu , hilo huenda likazua switofahamu katika mazungumzo ya mkufunzi mpya.

United inasema kwamba Woodward anaendelea na kazi yake na kwamba wana watu wengine , mpatanishi Matt Judge atakayeanza , ambaye anahusika na masuala ya uajiri . Lakini kwasasa Woodward na atakayemrithi Mkurugenzi Richard Arnold , wote wanahusishwa na waneleweka kuwasiliana na mwenyekiti Joel Glazer siku ya Jumamosi jioni wakati ilipoamuliwa kwamba Solskjaer atafutwa kazi baada ya timu hiyo kulazwa na Watford. Woodward alikuwa mtu aliyetoa habari mbaya binafsi na alikuwa mtu aliyemwambia Carrick kushikilia wadhfa huo kwa muda.

Kylian Mbappe na Mauricio Pochettino
Getty Images
Kylian Mbappe na Mauricio Pochettino

Je United inamtaka Pochettino?

Huku wale waliopo katika klabu ya United wakitetea utumizi wao wa naibu mkufunzi hadi msimu ujao wa joto, wanatambua kwamba iwapo kuna mtu ambaye yuko katika fikra zao kuchukua wadhfa huo kwa muda mrefu basi ni mkufunzi huyu.

Inajulikana kwamba Mkufunzi Mauricio Pochettino anapendelea wazo la kujiunga na United. Pia inafikiriwa kwamba Pochettino anaweza kusajiliwa hivi sasa iwapo United ingeshinikiza kumuajiri kutokana na hali ya mfumo unaomzunguka katika klabu ya PSG.

Maafisa wa United wamezungumza kwa kirefu kuhusu raia huyo wa Argentina kutokana na kazi nzuri aliofanya katika klabu ya Tottenham , hadi katika fainali ya kombe la klabuu bingwa Ulaya 2019.

Hivyobasi tunauliza ni mkufunzi yupi atakayeajiriwa na United?

Kawaida haijulikani ni nani huwa anafanya maamuzi makubwa ya klabu hiyo. Antonio Conte, ambaye aliihama Inter Milan msimu uliopita wa joto baada ya kushinda Seria A, hakuwa na kazi na alipatikana siku ambayo United walinyukwa bao 5-0 nyumbani na Liverpool Oktoba 24, kipigo ambacho wengi wanaamini kilichangia kutimuliwa kwa Solskjaer.

Badala yake walimdumisha Solskjaer naye Conte akajiunga na Tottenham.

Hisia zilikuwa ni kana kwamba Conte angekuwa mgumu sana kumsimamia na alama za mzozo na Jose Mourinho akiwa Old Trafford bado zipo.

Na pia hakuna kocha wa hadhi ya juu aliye rahisi kusimamia. Ferguson hakuna, Pep Guardiola la, Pochettino hata yeye sio rahisi.

Pochettino anahisi anaweza kupata nguvu zaidi za kuwaajiri wachezaji akiwa United kuliko anavyofanya Paris. Swali ni je United inaweza kumpa hilo mtu ambaye hajashinda taji Uingereza na aliiongoza PSG na kushindwa kupata Ligue 1 mara ya pili katika kipindi cha miaka tisa?

Vile vile kuna wengi ndani na nje ya Old Trafford, wanaohisi kuwa Pochettino atakuwa mtu bora - kwa sasa au msimu ujao. Lakini hakuna uteuzi unafanywa bila hatari.

Nani wa kuangaliwa pia?

Ikiwa kuna hatari upande wa Pochettino, kuna nyingi pia kwa watahiniwa wengine.

Brendan Rodgers amefanya kazi nzuri huko Leicester kwa misimu miwili, na kumaliza ndani ya nafasi tano za kwanza kwa miaka iliyofuatana na kushinda kombe la FA msimu uliopita.

Lakini ushindi wao dhidi ya United Oktoba 16 ni moja kati ya ushindi wa mechi nne katika mechi 15 kwenye mashindano yote.

Walikemewa wakati wa mapunziko Jumamosi waliposhindwa nyumbani na Chelsea, wako nafasi ya chini katika jedwali na wanahitaji kuwashinda Legia Warsaw Alhamisi ikiwa wana nia ya kufika awamu ya maondoano wa kombe la Yuropa.

Huko Ajax, Erik ten Hag amekuwa na jina zuri, kwa kukiongoza klabu hadi nusu fainali ya Champions League ambapo walikuwa na uhakika wa kufika fainali kabla ya matumaini yao kuzimwa na Tottenham.

Amefanikiwa kufanya hivyo licha ya kupoteza wachezaji wake mahiri akiwemo kiungo wa kati Danny van de Beek ambaye hakutumiwa sana na Solkjaer.

Lakini pengo kati ya Eredivisie na Ligi ya primia ni kubwa. Na kipindi chake Frank de Boer kilikumbwa na utata huko Cystal Palace hakitasaidia wakati United inatafakari kile meneja mholanzi anaweza kuwapa.

Zinedine Zidane anapatikana lakini hana nia ya katafuta kazi hiyo. Luis Enrique huenda asikaribishe kuzuizi chochote kwa maandalizi ya kupeleka Uhispania Kombe la Dunia na hatawaacha hadi mwishoni mwa mwaka ujao, isipokuwa tu aamue kuondoka hatua ambayo haitarajiwi.

"Inatia aibu sana", mshambuliaji wa zamani wa Celtic, Blackburn na Chelsea, Chris Sutton anasema akifananisha mikakati yao na klabu ya Stenhousemuir.

"Hiki ni klabu kinachodai kuwa klabu kubwa zaidi duniani na hawana mpango wa dharura. Kuna wasiwasi. "

Mlinzi wa zamani wa Manchester City Micah Richards ametaja hali iliyopo kuwa ya kama machafuko.

Ole Gunnar Solskjaer
Getty Images

"Hapa tunaizungumzia Manchester united, alisema Richard, Hawafanyi mambo kama klabu kubwa zaidi duniani.

Wako na mtu [Carrick] asiye na uzoefu katika uongozi, Inazidi kuwa mbaya zaidi.

Kipi kitafuata?

Vile Carrick alisema, lengo ni kwa mechi ya Champions League dhidi ya Villarreal ambapo United ni lazima ihakikishe haitashindwa ikiwa wanataka kusonga kwenda awamu ya muondoano.

Baada ya hapo ni mechi na Chelsea, mechi ambayo mashabiki wa United wataihudhuria kwa woga kutokana na kichapo ambacho tayari wamepata kutoka Liverpool na Manchester City.

Nyuma ya pazia harakati za kusaka meneja zinaendelea. Wadau wa ndani wanasisitiza kuwa wanafanya mpango licha ya hali kutoeleweka nje.