Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 11.06.2022: Milinkovic-Savic, Pogba, Zidane, Kounde, Jesus, Marquinhos

11 Junio, 2022

kiungo wa kati wa Lazio Mserbia Sergej Milinkovic-Savic,
AFP
Kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic,

Arsenal wako tayari kulipa zaidi ya pauni milioni 42 kwa ajili ya kiungo wa kati wa Lazio Mserbia Sergej Milinkovic-Savic, ingawa Newcastle wanaweza pia kuweza dau kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17. (Corriere dello Sport - in Italian)

PSG wanajaribu kumshawishi kocha wa zamani wa Real Madrid Zidane, 49, kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino kama meneja wao mpya. (ESPN)

P
Getty Images
Kiungoo wa kati Paul Pogba

Paul Pogba bado hajakamilisha mkataba wake wa uhamisho huru wa kutoka Man United kuelekea Juventus huku kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29, akisubiri kuona iwapo Zinedine Zidane anateuliwa kama kocha wa Paris St-Germain. (RMC Sport - in French)

Sevilla inasema kiungo wa safu ya kati-nyuma Mfaransa Jules Kounde anaangalia uwezekano wa kuondoka katika klabu hiyo msimu huu, huku Chelsea ikitarajiwa kusaini mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Sport Witness)

mshambuliaji Mbrazili wa Manchester City Gabriel Jesus
Getty Images
Mshambuliaji Mbrazili wa Manchester City Gabriel Jesus

AC Milan ndio klabu ya hivi karibuni kabisa kuonyesha nia ya kusaini mkataba na mshambuliaji Mbrazili wa Manchester City Gabriel Jesus, 25. (90min)

Arsenal wako tayari kutangaza kusaini mktaba na mshambuliaji mbrazili mwenye umri wa miaka 19, Marquinhos kutoka klabu ya Sao Paulo mkataba wa miaka mitano kwa malipo ya takriban pauni milioni 3. (Guardian)

b
Getty Images
Mchezaji wa Leeds United Raphinha

The Gunners ni miongoni mwa klabu zinazoangalia uwezekano wa kumchukua - mchezaji wa Leeds United Raphinha msimu huu, huku Barcelona, Manchester United, Chelsea na Liverpool zikihusishwa pia na winga huyo Mbrazili mwenye umri wa miaka 25. (Telegraph - subscription required)

Liverpool bado haijakubali gharama kwa ajili ya mshambuliaji wa Benfica, Darwin Nunez, blakini Muruguay huyo mwenye umri wa miaka 22t tayari amewaambia marafiki zake na familia yake kwamba anahamia Anfield. (Echo)

Lukaku
BBC
Lomelu Lukaku

Uhusiano wa mmiliki wa Chelsea Todd Boehly na Jay-Z's Roc Nation Sports unaweza kuwa ni muhimu kwa hali ya baadaye ya Romelu Lukaku, 29, na matumaini ya mshambuliaji huyo wa Ubelgiji ya kuhamia nter Milan. (Telegraph - subscription required)

Inter Milan bado hawajafanya mkataba wa moja kwa moja na Chelsea kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba na Lukaku. (Fabrizio Romano, Twitter)

Joao Palhinha wa Sporting Lisbon amesalia kuwa ndiye mchezaji anayelengwa zaidi na Wolves msimu huu licha ya nia ya Fulham kwa kiungo huyo wa safu ya kati wa Ureno, 26. (MailOnline)

Hellas Verona wakota yari kulipia gharama ya kumnunua mchezaji wa zamani aliyeajiriwa kwa mkopo Giovanni Simeone halafu wamuuze mshambuliaji Marhentina, huku West Ham na Arsenal zikiwa na nia na mchezaji huyo mwneye umri wa miaka 26, ambaye kwa sasa yuko katika klabu ya Cagliari. (AS - in Spanish)

Ainsley Maitland-Niles
BBC
Kiungo wa kati Ainsley Maitland-Niles

Klabu mpya iliyopandishwa daraja nchini Uingereza ya Nottingham Forest inamlenga kiungo wa kati wa Arsenal Muingereza Ainsley Maitland-Niles, 24, ambaye amekuwa akicheza kwa mkataba wa mkopo katika Roma msimu uliopita. (Mirror)

Tottenham wameafiki mkataba wa kumnunua mchezaji wa Middlesbroug Djed Spence, ambaye amekuwa akichea kwa mkataba wa mkopo katika klabu ya Forest msimu uliopita, huku gharama ya kiungo huyo wa nyuma-kulia mwenye umri wa miaka 21, rai awa Uingereza akifahamika kulipwa karibu pauni 20. (Guardian)

mshambuliajii Muingereza mwenye umri wa miaka 20- Cameron Archer
Getty Images
Mshambuliajii Muingereza mwenye umri wa miaka 20- Cameron Archer

Rangers inataka hadi pauni milioni 25 kwa ajili ya Calvin Bassey na Aston Villa wanaweza kumtumia mshambuliajii Muingereza mwenye umri wa miaka 20- Cameron Archer, ambaye alikuwa na mkataba wa mkopo na Preston lmsimu uliopita huku wataka kupanga mkataba mkataba kamili na mchezaji huyo wa huu la kushoto kutoka Nigeria akiwa na umri wa miaka 22. (Birmingham Mail)

Fulham wanakaribia kumalizia mkataba na mlindalango wa Lazio Malbania Thomas Strakosha, 27. (90min)

Wakala wa Miguel Almiron hadhani kwamba kiungo huyo wa kati wa Uruguay , 28, ataondoka Newcastle. (Chronicle Live)

Naby Keita
Getty Images
Kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita

Liverpool wameanza mazungumzo na Naby Keita juu ya mkataba kwa ajili ya kiungo huyu wa kati wa raia wa Guinea, 27. (Football Insider)

Manchester United walitoa ofay a mkataba mpya kwa Martin Svidersky lakini kiungo huyo wa kati wa timu ya Slovakia ya vijana walio chini ya umri wa miaka 21, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 19 bado anataka kuondoka. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale anasema kuwa atajiunga na Getafe baada ya kuondoka Real Madrid msimu hu una mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 atafanya uamuzi juu ya hali yake ya baadaye baada ya mwisho wa Ligi ya nchi yake (The Athletic)