Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 08.06.2022: Mane, Saka, Tchouameni, Rashford, Eriksen, Nunez

08 Junio, 2022

Sadio mane
BBC

Liverpool wamekataa ofa ya £30m kwa mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane kutoka Bayern Munich.

The Reds wamepigwa na butwaa baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kurejea na ofa hiyo baada ya ofa ya awali, iliyoripotiwa kuwa na thamani ya hadi £25m, kukataliwa.

mshambuliaji wa Arsenal na England Bukayo Saka
Reuters
mshambuliaji wa Arsenal na England Bukayo Saka

Manchester City wamekataa taarifa kwamba wanajiandaa kumchukua mshambuliaji wa Arsenal na England Bukayo Saka, 20. (Mirror)

Real Madrid wamekubaliana mkataba wenye thamani ya euro milioni 100 (£85m) na Monaco kwa ajili ya kiungo wa kati Mfaransa Aurelien Tchouameni. (Athletic)

mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford
Reuters
Mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford

Tottenham wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, 24, kwa ajili ya kuhamia katika klabu hiyo iliyopo kaskazini mwa London. (Caught Offside)

AC Milan wana matumaini ya kukamilisha kusaini mkataba na mlinzi Mholanzi Sven Botman, 22, na kiungo wa kati wa Ureno Renato Sanches, 24, kutoka Lille. (90min)

mshambuliaji wa Benfica na Uruguay Darwin Nunez
BBC
Mshambuliaji wa Benfica na Uruguay Darwin Nunez

Manchester United na Newcastle kwa pamoja zinaripotiwa kukaribia kabisa kusiani mkataba na mshambuliaji wa Benfica na Uruguay Darwin Nunez mwenye umri wa miaka 22. (Sebastian Giovanelli via Star)

Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel ameahidiwa na mmiliki wamklabu hiyo Todd Boehly kuwa anaweza kuongoza kazi ya uhamisho katika hatua iliyopangwa ya kuimarisha kikosi kipya cha Manchester City na Liverpool. (Telegraph - subscription required)

Kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma
Getty Images
Kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma

Kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma, 25, hayuko tena katika orodha ya wachezaji wanaopangwa kuchukuliwa na Aston Villa. Hatahivyo, meneja wa Villa Steven Gerrard anaweza kuendelea bado kumtafuta kiungo wa kati msimu huu. (Athletic)

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 33, alikiambia kipindi cha matangazo ya mtandaoni (podcast) kwamba anaondoka ayern Munich kwasababu anataka "hisia zaidi" katika maisha yake na machampioni hao wa Ujerumani "hawakutaka kunisikiliza hadi mwisho". (Bild - in German)

kiungo wa kati wa Denmark na Brentford Christian Eriksen
Getty Images
Kiungo wa kati wa Denmark na Brentford Christian Eriksen

West Ham wametuma kikosi cha kumfuatilia kiungo wa kati wa Denmark na Brentford Christian Eriksen, 30, p pamoja na mchezaji mwenzake wa kimataifa , kiungo wa nyuma-kulia wa Atalanta Joakim Maehle, 25, katika mchezo wa Ligi ya taifa utakaochezwa Jumatatu kwa mtazamo wa kuwahamisha wachezaji hao wawili. (Star)

Leeds United wamejiunga na Southampton pamoja na West Ham katika nia yao ya kumnunua mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Austria Junior Adamu mwenye umri wa miaka 20. (Sky Sports Austria)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Uholanzi Robin van Persie,
BBC
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Uholanzi Robin van Persie,

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Uholanzi Robin van Persie, 38, anasema kuwa alikataa fursa ya kujiunga na Erik ten Hag kama kocha msaidizi katika Old Trafford. (Mirror)

Barcelona wako tayari kwa mazungumzo na Manchester United kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Mholanzi Frenkie de Jong, 25, kuelekea Old Trafford lakini klabu hiyo ya Uhispania bado haijapokea ofa rasmi kutoka United. (Sport - in Spanish)