Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 06.06.2022: Salah, Spence, Gavi, Matic, Luiz

06 Junio, 2022

Sala
Getty Images

Barcelona wamemwambia mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah, 29, kwamba anaweza kujiunga nao kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake na Reds utakapomalizika msimu ujao. (Mirror)

Tottenham wanajiandaa kuongeza juhudi za kumsaka beki wa Middlesbrough Muingereza Djed Spence, 21, ambaye alikuwa Nottingham Forest kwa mkopo wa msimu mzima. (Express)

Liverpool wamemaliza nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona mwenye umri wa miaka 17 raia wa Uhispania Gavi. (Sport - kwa Kihispania)

Kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic, 33, atajiungfa na Roma kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wake utakapomalizika Manchester United mwisho wa mwezi huu wa Juni. (Sky Sports)

Roma inaweza kusitisha juhudi za kumsaka Matic ikiwa itafanikiwa kumnunua kiungo wa kati wa Aston Villa na Brazil Douglas Luiz, 24. (Barua ya Birmingham)

Benfica wana matumaiani ya kufikia makubalianao na mchezaji wa kimataifa wa zamani wa Ujerumani Mario Gotze, 30, kuhusu uhamisho kutoka PSV. (Fabrizio Romano)

Mario Gotze in action for Borussia Dortmund
Getty Images

Chelsea huenda ikasaidia kumshawishi mchezaji wao Declan Rice, 23, kurejea nyumbani kutoka klabu ya West Ham kwa kumpatia kiungo huyo wa kati wa Uingereza fulana nambari 41 mgongoni. (Express)

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Mateu Alemany anatazamiwa kuruka kuelekea Uingereza wiki hii kuanza mazungumzo na Leeds kuhusu mpango wa kumnunua fowadi wa Brazil Raphinha, 25. (Sport, via Mail).

Beki wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 22, amethibitisha kuwa yuko kwenye mazungumzo na Juventus kuhusu mkataba mpya lakini bado hajajitolea kufanya uamuzi. (Dakika 90)

Matthijs De Ligt
Getty Images
Beki wa Uholanzi Matthijs de Ligt

Newcastle wamemfanya mlinzi wa Atletico Madrid raia wa Brazil Renan Lodi, 24, kuwa chaguo lao la kwanza kuziba pengo la beki wa kushoto. (Jacque Talbot, kupitia Give Me Sport)