Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 04.06.2022: Raphinha, Kane, Lukaku, Bergwijn, Chiellini, Bissouma, Cavani

04 Junio, 2022

Mshambuliaji wa Liverpool Msenegal Sadio Mane
Getty Images
Mshambuliaji wa Liverpool Msenegal Sadio Mane

Mshambuliaji wa Liverpool Msenegal Sadio Mane, 30, anasema atafanya kile ambacho watu wanataka alipokuwa akijibu kuhusu kura ya maoni nchini Senegal ambayo ilibaini kuwa 60-70% ya watu wanamtaka oondoke Liverpool . (Sky Sports)

Leeds United haitakubali dau la chini ya pauni milioni 60 kwa ajili ya winga wa Brazil Raphinha, 25, wambaye amekuwa akihusishwa sana na taarifa za kuhamia Barcelona. (The Athletic - subscription required)

Mshambuliaji wa Tottenham na nahodha wa England Harry Kane
Getty Images
Mshambuliaji wa Tottenham na nahodha wa England Harry Kane

Mshambuliaji wa Tottenham na nahodha wa England Harry Kane, 28, sasa anaweza kusaini mkataba mpya wa kubakia katika klabu hiyo. (Express, via GiveMeSport)

Manchester United wametoa ofa kwa mlinzi Muingereza Wan-Bissaka,
Getty Images
Manchester United wametoa ofa kwa mlinzi Muingereza Wan-Bissaka,

Manchester United wametoa ofa kwa mlinzi Muingereza Wan-Bissaka, 24, ya walau klabu moja na pia wanataka kumuuza mlinzi wa England , kikosi cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Brandon Williams. (Manchester Evening News)

Winga wa Tottenham Mholanzi Steven Bergwijn, 24, anasakwa na klabu ya Ajax, ambao wako tayari kumpatia mchezaji huyo wa zamani wa PSV Eindhoven mkataba mpaka mwaka 2027. (De Telegraaf - in Dutch, subscription required)

Winga Mbelgiji wa klabu ya Chelsea Romelu Lukaku, 29
BBC
Winga Mbelgiji wa klabu ya Chelsea Romelu Lukaku

Winga Mbelgiji wa klabu ya Chelsea Romelu Lukaku, 29, iyuko tayari kuchukua malipo yaliyopunguzwa ili aweze kurejea tena katika Inter Milan, miezi 10 baada ya kuondoka kwenye klabu hiyo kujiunga na the Blues kwa rekodi ya pauni milioni 97.5 . (Telegraph - subscription required)

Tottenham na Chelsea wanashindania kusaini mkataba na mlinzi wa klabu za RB Leipzig Croatia Josko Gvardiol, 20. (Mail)

mshambuliaji Mbelgiji Divock Origi
Getty Images
Mshambuliaji Mbelgiji Divock Origi

AC Milan wanajiandaa kutangaza kusaini mkataba namshambuliaji Mbelgiji Divock Origi, 27, ambaye amekwishaaga katika Liverpool. (Fabrizio Romano, Twitter)

Aston Villa wanakamilisha taratibu za kusiani mkataba wa £2.8m kutoka kwa mlindalango wa Roma Mswidi Robin Olsen, 32, baada ya msimu wake wa mkopo kuisha msimu uliopita. (Mail)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Mfaransa Corentin Tolisso, 27, anaweza kuhamia katika Primia Ligi wakati mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa mwezi Juni . (ESPN)

mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini
Getty Images
Mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini

Mchezaji mwenye uzoefu wa Juventus na mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini, 37, yuko tayari kuhamia Marekani kusiani mkataba na Los Angeles FC. (Sky Sports Italia)

Brentford wanajiandaa kumnunua mshambuliaji wa Watford Mnigeria Emmanuel Dennis mwenye umri wa miaka 24 kwa pauni milioni 20. (Sun)

kiungo wa kati wa Brighton Yves Bissouma,
Getty Images
Kiungo wa kati wa Brighton Yves Bissouma

Monaco itajaribu kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Brighton Yves Bissouma, 25, kama mchezaji mvbadala wa kiungo wa kati wa Ufaransa Aurelien Tchouameni, 22, ambaye anaondoka. Tchouameni amezivutika klabu za Real Madrid, Paris St-Germain na Liverpool. (Talksport)

Klabu ya Italia Salernitana ina nia ya kusiani mkataba na mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 35, ambaye anatafuta klabu mpya baada ya kuondoka katika Manchester United. (Mail)

Bournemouth lazima wailipe Liverpool £15m iwapo watataka kuugeuza uhamisho wa mkopo Nathaniel Phillips kuwa mkataba wa kudumu. Mlinzi huyo Muingereza mwenye umri wa miaka 17 alicheza mechi 17 katika klabu ya Cherries msimu uliopita, akiwasaidia kushinda kuinuliwa daraja na kuingia Primia Ligi . (Liverpool Echo)