Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 02.06.2022: Salah, Mane, Kounde, Ekitike, Pogba, De Jong, Keita, Palhinha

02 Junio, 2022

TH
Getty Images

Mshambulizi wa Liverpool kutoka Misri Mohamed Salah, 29, angependelea kujiunga na timu pinzani ya Ligi Kuu msimu ujao ikiwa hakuna mkataba mpya wa kusalia Reds utakaokubaliwa. (The Athletic - subscription required)

Mshambulizi wa Senegal Sadio Mane, 30, anataka kuondoka Liverpool msimu huu wa joto, huku klabu ya Bayern Munich ikiwa na ushindani mkubwa katika kuiwania saini yake. . (Fabrizio Romano, Twitter)

Chelsea wameanza mazungumzo na Sevilla kuhusu kumsajili beki wa Ufaransa mwenye thamani ya pauni milioni 50 Jules Kounde, 23, ambaye aliisaidia klabu hiyo ya Uhispania kushinda Ligi ya Europa mwaka 2020. (Sport - in Spanish)

Newcastle wako kwenye majadiliano juu ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Reims mwenye umri wa miaka 19 Mfaransa Hugo Ekitike katika mkataba wa pauni milioni 25 pamoja na zaidi. (Daily Mail's Craig Hope, Twitter)

th
Getty Images

Baada ya kutangaza kuachana na Paul Pogba na Jesse Lingard, Manchester United imeanza mazungumzo na Barcelona kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, kuhusu uhamisho wa £72.5m kwenda Old Trafford. (Fabrizio Romano, Twitter)

Lakini United watatafuta kumnunua kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27, kama mbadala wa De Jong. (GiveMeSport)

Juventus wana imani kwamba wamekubali mpango wa kumrejesha Pogba, 29, wakati mkataba wa kiungo huyo wa kati wa Ufaransa na Manchester United utakapokamilika msimu huu. (90min)

Liverpool wanapanga kumpa kiungo wa Guinea Naby Keita, 27, mkataba mpya. Paris St-Germain wanamtaka mchezaji huyo lakini Reds wanatumai kusalia Keita hadi msimu ujao wa joto wakati mkataba wake wa sasa utakapomalizika. (The Athletic - subscription required)

Wolves wanakaribia kumsajili Joao Palhinha wa Sporting Lisbon, huku kiungo huyo wa kati wa Ureno, 26, akikubali kujiunga kwa mkataba wa muda mrefu kwa ada ya takriban £20m. (Sun)

Manchester City wanasalia kumtaka kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 26, lakini Leeds United bado wana matumaini ya kumbakisha mchezaji huyo baada ya kuepuka kushushwa daraja. (Sun)

Real Madrid wanamtaka kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham, lakini hawatamnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 hadi 2023. (Bild - in German)

Bayern Munich watajaribu kumsajili fowadi wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, ambaye anasakwa na Inter Milan(GiveMeSport)

th
Getty Images

Manchester United wamemtanguliza mlinzi wa Ajax na Uholanzi Jurrien Timber, 20, lakini pia wamefanya duru mbili za mazungumzo na mlinzi wa Braga Mreno David Carmo, 22. (Manchester Evening News)

Beki aliyeshuka daraja wa Burnley wa Uingereza James Tarkowski, 29, anasakwa na Aston Villa, Everton, West Ham, Newcastle na Fulham. .(Mirror)

Villarreal wapo kwenye mazungumzo ya juu ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Giovani lo Celso kwa mkataba wa kudumu kutoka Tottenham. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na klabu hiyo ya Uhispania kwa mkopo mwezi Januari. (Football Insider)

Aston Villa wanataka wachezaji wengine watatu baada ya kumuongeza kiungo wa kati Mfaransa Boubacar Kamara, 22, kutoka Marseille, beki wa kati wa Brazil Diego Carlos, 29, kutoka Sevilla na kubadilisha uhamisho wa mkopo wa fowadi wa Brazil Philippe Coutinho, 29, kutoka Barcelona kuwa usajili wa kudumu. Mshambulizi wa Uruguay mwenye umri wa miaka 35, Luis Suarez, ambaye anaondoka Atletico Madrid, ni mmoja wa wale wanaozingatiwa. (The Athletic - subscription required)