Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 29.05.2022: Kante, Dembele, Dybala, Di Maria, Gallagher, Perisic, Raphinha, Gundogan

29 Meyo, 2022

Edinson Cavani
Getty Images
Edinson Cavani

Mshambulizi wa Uruguay Edinson Cavani, 35, anasema amesalia na "ladha chungu" katika barua ya wazi kwa Manchester United baada ya kuondoka katika klabu hiyo. (Star)

Liverpool wamefanya mawasiliano na winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 25, ambaye mkataba wake wa Barcelona unaisha msimu huu wa joto(Sport - in Spanish)

Manchester United wanafikiria kuwasilisha ombi la kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 31(Guardian)

th
Getty Images

Mkufunzi wa Chelsea Thomas Tuchel atafanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 22, kabla ya kuamua mustakabali wake. Msimu uliopita alicheza kwa mkopo Crystal Palace. Fabrizio Romano)

Mchezaji mwingine ambaye anatazamiwa kuzungumzia nafasi yake ni kiungo wa kati wa Manchester City Mjerumani Ilkay Gundogan, 31(90min)

Mkufunzi mtarajiwa wa Burnley Vincent Kompany anataka kumfanya beki wa kati Muingereza Taylor Harwood-Bellis, 20, kuwa usajili wake wa kwanza Turf Moor kwa mkopo kutoka klabu ya zamani ya Manchester City. (TSun)

Winga wa Croatia Ivan Perisic, 33, anatazamiwa kusaini mkataba wa kujiunga na Tottenham Hotspur kutoka Inter Milan kwa uhamisho wa bure na mpango huo unaweza kutangazwa wiki ijayo. (Fabrizio Romano)

th
Getty Images

Mkufunzi wa Roma Jose Mourinho anatumai kushinda vilabu vya zamani vya Tottenham na Manchester United katika kumsajili mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 28, kwa uhamisho wa bure baada ya kuondoka Juventus msimu huu wa joto. (TyC Sports, via Express)

Paris St-Germain wanataka kumsajili mshambuliaji wa Brazil Richarlison, 25, kutoka Everton msimu huu wa joto. (Fichajes - in Spanish)

Babake winga wa Leeds Raphinha anasema "uwezekano upo" juu ya mustakabali wake huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 akiendelea kuhusishwa na Barcelona. (Express)

th
Getty Images

Juventus wamempa mkataba wa mwaka mmoja winga wa Argentina Angel di Maria, 34, baada ya kuamua kuondoka PSG mwishoni mwa msimu huu. (Calciomercato - in Italian)

Beki wa Kijapani wa Manchester City Ko Itakura, 25, anavutiwa na Bournemouth na Fulham baada ya muda mzuri wa mkopo katika klabu ya Schalke. (Sky Sports)