Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 06.04.2021: Haaland, Sancho, Messi, Salah, Ibrahimovic, Foyth

06 Abril, 2021

Erling Braut Haaland
Getty Images
Wakala wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland amepinga tetesi za uhamisho wake

Wakala wa mchezaji Erling Haaland, Mino Raiola amekana tetesi kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland,20. (Goal)

Mtendaji Mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke amesisitiza kuwa klabu yake inataka kumfanya Haaland awe na furaha zaidi klabuni hapo ili aweze kusalia mpaka msimu ujao. (Dazn via Mirror)

Hatahivyo Mtendaji huyo mkuu wa Borussia , anasema klabu hiyo itasikiliza ofa kwa ajili ya winga wa England Jadon Sancho. (Manchester Evening News)

Winga wa England Jadon Sancho
Getty Images
Winga wa England Jadon Sancho

Kocha Pep Guardiola amesema Manchester City wanaweza kuamua kutumia zaidi ya pauni milioni 100 kwa ajili ya mchezaji mmoja siku za usoni, lakini ameendela kuwa na kigugumizi juu ya tetesi kuhusu klabu yake kuhusishwa na Haaland. (Sky Sports)

Barcelona itaendelea na mipango yake ya kumuwania Mshambuliaji wa Borrusia Haaland raia Norway baada ya kukutana na wawakilishi wake wiki iliyopita, lakini vyanzo katika klabu hiyo wanasema kuwa itakuwa''vigumu sana'' kutekeleza azma yao. (ESPN)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amevunja ukimya ukimya kuhusu tetesi za uhamisho zinazomuhusisha mshambuliaji wa Misri na Liverpool Mohamed Salah,28, kuhamia Bernabeu. (Liverpool Echo)

Mohamed Salah
Getty Images
Je mshambuliaji wa Misri na Liverpool Mohamed Salah atahamia Real Madrid?

Villarreal wana matumaini ya kumsajili mlinzi Juan Foyth,23, wa Tottenham msimu huu kwa mkataba wa kudumu kwa kiasi cha chini ya ada ya pauni milioni 13.Kwa sasa mchezaji huyo anacheza kwa mkopo katika klabu hiyo.(Football Insider)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Angel di Maria, 33, amesema itakuwa ''vizuri sana'' kucheza na Muajentina mwenzake Lionel Messi,33, wakati kukiwa na mashaka kuhusu mustakabali wake ndani ya Barcelona. (AS)

Mmiliki wa zamani wa As Roma James Pallotta ameeleza shauku yake ya kutaka kuinunua klabu ya Newcastle United ya nchini England (The Athletic)

Di Maria
Getty Images
Mchezaji wa PSG Angel di Maria amesema itakuwa ''vizuri sana'' kucheza na Muajentina mwenzake Lionel Messi

Mshambuliaji Ac Milan Zlatan Ibrahimovich, 39, anatarajia kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na AC Milan. (Sky Sports)

Norwich City itamtunza raia wa Norway Alex Tettey chochote kile kuhusu mustakabali wake kiungo huyo wa miaka 35 Tettey amekuwa Norwich tangu 2012 na mkataba wake unamalizika msimu wa joto. (Norwich Evening News)