Chelsea VS West Brom: Baggies wavunja rekodi ya Blues ya kutofungwa katika mechi 14

03 Abril, 2021

Matheus Pereira (left)
EPA
Chelsea hawajawahi kufungwa mabao matano nyumbani tangu Oktoba mwaka 2011 walipofungwa kwa 5-3 na Arsenal

Matheus Pereira na Callum Robinson walifunga mara mbili wakati West Brom ambayo imekuwa ikijikokota katika Ligi Kuu ya Uingereza ilipoizidi nguvu kikosi cha Chelsea cha wachezaji 10- kuvunja rekodi yao ya kutoshindwa katika mechi 14 mfululizo chini ya ukufunzi wa Thomas Tuchel, Stamford Bridge.

Baggies walionesha mchezo mzuri sawa na Blues, ambao walikuwa wamekosa huduma ya Thiago Silva aliyetupwa nje ya uwanja katika dakika 29.

Wachezaji wa Sam Allardyce walionesha ujuzi wao katika safu ya mashambulizi na kila bao walilofunga lilikuwa la hali ya juu.

Chelsea waliongoza katika dakika ya 27. Hata hivyo dakika mbili baadaye hali yao ilianza kubadilika na kuwa mbaya zaidi wakati Thiago alipooneshwa kadi ya njano kwa mara ya pili.

Chelsea and West Brom players
PA Media
Wachezaji wa Chelsea na West Brom

Hii ni mara ya kwanza tangu mwezi Oktoba mwaka 2011 kwa Chelsea kufungwa mabao matano nyumbani, walipofungwa kwa 5-3 na Arsena.

Matokeo haya yanamaanisha Chelsea bado wanasalia nafasi ya nne katika jedwali la msimamo wa Ligi ya EPL nao West Brom wakiwa nafasi ya 19

Je! Hii ilikuwa kosa la kiufundi ya Thomas Tuchel?

Hatua yake ya kuwacha nje baadhi ya wachezaji wake wa mara kwa mara wa kikosi cha kwanza, wakiwemo Mount na Kai Havertz, ni kwa sababu alitaka miguu safi kabisa uwanjani kwa sababu ya bidii ya wachezaji wake wa benchi wakati wa mapumziko ya kimataifa.

Wale walioanza huenda walikuwa sawa, lakini walikuwa wazito nyakati zingine hali iliyomfanya Thiago kufanya kazi ya ziada na hatimaye kujipata mashakani.

wachezaji wa West Brom
Reuters

Ilikuwa hatari kumchezesha MBrazil huyo mwenye umri wa miaka 36, ambaye haJAkuwa uwanjani kwa miezi miwili baada ya kujeruhiwa. Aliimarisha mchozo wa timu yake lakini hata kama alipewa kadi ya kwanza ya njano lakini kadi ya pili haikutarajiwa kwa mchezaji wa kiwango chake.

Dane Andreas Christensen, ambaye alichukuwa nafasi ya Thiago, kushirikiana na mkiungo wa kati Hakim Ziyech kutoa nafasi zaidi.

Mshambuliaji Timo Werner aliingia uwanjani lakini utenda kazi wake pengine ungelifua dafu laiti angelikchukua maamuzi ya haraka kama ya Pulisic kuipatia bao timu yake, japo alimsaidia Mount kufunga bao

Yeye pamoja na wachezaji wenzake huenda wanatamani wangelikuwa nje katika mechi za kimataifa.

Chelsea wana siku nne kujiondolea fedheha ya leo watakapokutana na Porto katika robo fainali ya Champions League.

Sam Allardyce
Reuters
Hii ni mara West Brom ufunga mabao matano ugenini katika Ligi Kuu England - mara ya mwisho walifanya hivyo dhidi ya Wolves Februari 2012 (5-1)