Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 14.01.2021: Lingard, Trippier, Balogun, Rose, Ozil, Garcia

14 Ene, 2021

Jesse Lingard
Getty Images
Kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard

Wawakilishi wa kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28, wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu uhamisho wake wa mkopo kwenda Nice, lakini mazungumzo rasmi yakitarajiwa kufanyika wiki ijayo. (Sky Sports)

Meneja wa Newcastle Steve Bruce anauungwaji mkono wa mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley, licha ya shinikizo kutoka kwa mashabiki wanaotaka afutwe kazi baada ya kushindwa despite na Sheffield United kati kati ya wiki. (Sky Sports)

Manchester United wamesitisha mpango wa kumnunua mchezaji wa Atletico Madrid wa safu ya kulia na kushoto Muingereza Kieran Trippier, 30, mwezi huu huku kukiwa na wasiwasi kuhusu matokeo ya marufuku ya kimataifa dhidi yake kwa kukiuka sheria ya kucheza kamari. (Manchester Evening News)

Kieran Trippier
Getty Images
Manchester United yamesitisha mpango wa kumnunua Kieran Trippier kutoka Atletico Madrid

Tottenham huenda ikafutilia mbali mkataba wa Danny Rose katika dirisha la uhamisho wa Januari, huku West Brom ikionesha azma ya kutaka kumnunua beki huyo aliye na umri wa miaka 30. (Talksport)

Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil, 32, ameamua kuacha £7m alizotarajiwa kupokea kabla ya mwisho wa msimu huu ili afanikiwe kukatiza mkataba wake na kuondoka mwezi huu. (The Athletic)

Danny Rose
Getty Images
Beki wa Tottenham Danny Rose

Mlinzi wa Manchester City ana Uhispania Eric Garcia, 20, amefikia makubaliano ya kibinafsi na Barcelona, lakini uhamisho wake haujakaribia kukamilika. (Goal)

Meneja wa Barcelona Ronald Koeman ana imani ya kuwasajili kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, na mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 26 kwa mkopo msimu huu. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Liverpool Georginio Wijnaldum
Getty Images
Kiungo wa kati wa Liverpool Georginio Wijnaldum

Mshambuliaji wa Arsenal Muingereza Folarin Balogun, 19, amekubali kujiunga na RB Leipzig. (Football Insider)

Liverpool wanajiandaa kumnunua mlinzi wa Brighton Muingereza Ben White, 23. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa zamani wa England Jack Wilshere, 29, amemvutia kocha wa Bournemouth Jason Tindall na huenda akapata mkataba wa muda mfupi na klabu hiyo. (Mail)

Kiungo wa kati wa zamani wa England na West Ham Jack Wilshere
Getty Images
Kiungo wa kati wa zamani wa England na West Ham Jack Wilshere

Meneja wa Tottenham Jose Mourinho anasisitiza kuwa kiungo wa kati wa England Harry Winks, 24, hatauzwa au kutolewa wa mkopo mwezi huu. (Football London)

Beki wa Everton Jonjoe Kenny huenda akaondoka klamu hiyo katika dirisha la uhamisho la Januari, na Burnley wameonesha azma ya kutaka kumnunua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23. (Liverpool Echo)

Tetesi za soka Ulaya Jumatano

Kiungo wa kati Fernandinho, 35, huenda akaongeza kandarasi yake katika klabu ya Manchester City kwa kuwa hana uhakikia iwapo akubali ofa kutoka Ulaya na Marekani ya latini wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu wa joto. (Telegraph - subscription required)

Fernandinho
BBC

Beki wa Napoli Kalidou Koulibaly - amehusishwa pakubwa na uhamisho wa Liverpool, Manchester City na Manchester United - atauzwa katika dirisha la uhamisho la mwezi huu iwapo timu itatoa ofa ya £100m kumnunua mchezaji huyo wa senegal mwenye umri wa miaka 29. (Talksport)

Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho amemshutumu kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil kwamba angependelea kustaafu badala ya kuichezea klabu ya Tottenham. Mourinho alisema kwamba asingemtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka. (The Sun)

Arsenal midfielder Mesut Ozil
Getty Images

Klabu ya AC Milan inataka kumsaini beki wa kati wa Chelsea Fikayo Tomori kwa mkopo katika kipindi cha msimu kilichosalia (The Guardian)

Real Madrid inapanga kuwauza wachezaji sita msimu huu ili kuchangisha fedha za kumsaini mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe, 22. Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, beki wa kushoto wa Brazil Marcelo, Mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic na wachezaji watatu wa Uhispania Isco, Dani Ceballos na Brahim Diaz ndio wachezaji wanaolengwa. (AS - in Spanish)

Kylian Mbappe
AFP
Mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anafiikria kumrudisha meneja wa zamani Avram Grant katika uwanja wa Stamford Bridge ili kumsaidia mkufunzi Frank Lampard. (Sky Sports)