Tetesi za soka Ulaya 13.01.2021: Mbappe, Fernandinho, Koulibaly, Ozil, Tomori

14 Ene, 2021

Avram Grant
Getty Images

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anafiikria kumrudisha meneja wa zamani Avram Grant katika uwanja wa Stamford Bridge ili kumsaidia mkufunzi Frank Lampard. (Sky Sports)

Real Madrid inapanga kuwauza wachezaji sita msimu huu ili kuchangisha fedha za kumsaini mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe, 22. Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, beki wa kushoto wa Brazil Marcelo, Mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic na wachezaji watatu wa Uhispania Isco, Dani Ceballos na Brahim Diaz ndio wachezaji wanaolengwa. (AS - in Spanish)

Beki wa Manchester United Timothy Fosu-Mensah, 23, anatarajiwa kuhamia katika klabu ya Bayer Leverkusen kwa dau la £1.5m baada ya kukataa kuongezewa mkataba katika uwanja wa Old Trafford. (Manchester Evening News)

Timothy Fosu-Mensah
Getty Images
Timothy Fosu-Mensah

Wolves haitamnyatia mshambuliaji anayelengwa na kocha Nuno Espiroto Olivier Giroud na yule wa Liverpool Divock Origi, 25, baada ya klabu hiyo kumwambia kocha huyo kwamba haina fedha za kutumia Januari. (Mirror)

Bayern Munich inatarajiwa kumsaini beki wa Reading mwenye umri wa miaka 22 Omar Richards kwa mkataba usio rasmi wakati ambapo inasubiri kandarasi yake kukamilika katika msimu wa joto.. Everton na West Ham zilikuwa na hamu ya kumsajili. (Guardian)

Kiungo wa kati Fernandinho, 35, huenda akaongeza kandarasi yake katika klabu ya Manchester City kwa kuwa hana uhakikia iwapo akubali ofa kutoka Ulaya na Marekani ya latini wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu wa joto. (Telegraph - subscription required)

Fernandinho
BBC

Beki wa Napoli Kalidou Koulibaly - amehusishwa pakubwa na uhamisho wa Liverpool, Manchester City na Manchester United - atauzwa katika dirisha la uhamisho la mwezi huu iwapo timu itatoa ofa ya £100m kumnunua mchezaji huyo wa senegal mwenye umri wa miaka 29-.. (Talksport)

Kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 28, ana thamani ya juu zaidi ya mchezaji yeyote yule wa Real Madrid kulingana na ripoti ya wataalamu wa ukaguzi. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Beki wa kushoto wa Barcelona Junior Firpo anatarajiwa kusalia katika klabu hiyo ya Nou Camp wakati wa dirisha hili la uhamisho licha ya hamu ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka. (Marca)

Casamiro
Getty Images

Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho amemshutumu kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil kwamba angependelea kustaafu badala ya kuichezea klabu ya Tottenham. Mourinho alisema kwamba asingemtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka. (The Sun)

Klabu ya AC Milan inataka kumsaini beki wa kati wa Chelsea Fikayo Tomori kwa mkopo katika kipindi cha msimu kilichosalia (The Guardian)

Mshambuliaji wa Leicester City na Algeria Islam Slimani, 32, anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa matibabu katika klabu ya Lyon na Ufaransa. (Sky Sports)

Tottenham, Sheffield United, Rangers na Celtic wote wanamnyatia mshambuliaji wa Wigan mwenye umri wa miaka 19 Kyle Joseph. (Mirror)