Tetesi za Soka Ulaya Jumanne tarehe 14.06.2022: Phillips, De Jong, Richarlison, Nkunku, Botman, Leno, Heaton, Choudhury

14 Junio, 2022

Frenkie de Jong
Getty Images

Manchester United imeanza mazungimzo na Barcelona kwa ajili ya usajili wa kiungo wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, lakini hawatataka kulipa fedha kubwa kupita kiasi wakati huu klabu hiyo ya Hispania ikitaka £85.7m. (Manchester Evening News)

Tottenham inataka kumsajili mshambuliaji wa Everton na Brazil Richarlison, the Toffees ikitaka ada ya £50m kwa ajili ya mbrazil huyo mwenye miaka 25. (Telegraph, subscription required)

Liverpool na Manchester City wanamfuatilia kiungo wa Barcelona na Hispania Gavi,17 ingawa ada ya uhamisho wake kwenye mkataba imefikia £85.7m. (Marca)

Manchester City inamtaka kusajili huku kiungo wa Leeds United na England Kalvin Phillips, 26, akionekana kuwindwa na mabingwa hao wa ligi kuu England. (Times, subscription required)

RB Leipzig inamuuza kwa ada ya £100m mshambuliaji wake mfaransa Christopher Nkunku, 24 huku Manchester United, Arsenal na Paris St-Germain zikionyesha nia ya kumtaka. (Independent

Christopher Nkunku
Getty Images
Christopher Nkunku

Newcastle United inatarajia kusaka mchezaji mwingine baada ya Lille kupandisha dau la mlinzi mholanzi Sven Botman, 22 kutoka £30m mpaka £36m. (Telegraph, subscription required)

Fulham inamtaka kipa wa Arsenal na Ujerumani Bernd Leno, 30, wakijiandaa kufanya vyema baada ya kurejea ligi kuu England. (Evening Standard)

Brighton inamsaka mlinzi wa kushoto wa Porto na Nigeria Zaidu Sanusi, 25, katika uhamisho utakaomruhusu nyota wa kimataifa wa Hispania Marc Cucurella, 23, kujiunga na Manchester City. (Daily Star)

Middlesbrough inamtaka kwa mkopo kipa wa Manchester United na England Tom Heaton, 36, na kiungo wa Leicester City muingereza Hamza Choudhury, 24. (Northern Echo)

Heaton
Getty Images
Tom Heaton

Leeds United wako katika hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho wa kiungo mhispania wa Bayern Munich Marc Roca, 25. (90min)

Swansea City, Middlesbrough, Preston na QPR zote zinamuwania kwa mkopo mshambuliaji wa Tottenham na Jamhuri ya Ireland, Troy Parrott, 20, kwa ajili ya msimu ujao wa 2022-23. (Football.London)

Coventry City imekataa ombi la Middlesbrough kwa ajili ya mshambuliaji Viktor Gyokeres, huku Fulham wakionekana kumtaka pia nyota huyo mwenye miaka 24. (Football Insider)