Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 08.04.2021: Lingard, Zaha, Sterling, Messi, Lukaku, Haaland, Konate, Vestergaard

08 Abril, 2021

Jesse Lingard
Getty Images
Kiungo wa kati wa Manchester United, Jesse Lingard

West Ham itafanya vyovyote vile ili kumnasa kiungo wa kati Jesse Lingard, 28, anayekipiga Manchester United. (Sky Sports)

Thamani ya Lingard kwa mujibu wa Manchester United ni pauni milioni 30. (Mirror)

Arsenal imerejesha nia yao tena kwa mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha,28. (90min)

Wilfried Zaha
Getty Images
Arsenal wameanza tena kumsaka mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha

Manchester City wanalenga kukubaliana kuingia mkataba mpya nawashambuliaji wa England Phil Foden,20, na Raheem Sterling,26, kabla ya mwishoni mwa msimu, baada ya kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne,29, kuongeza mkataba wake wa mpaka mwaka 2025. (Eurosport)

Manchester City haitamfuatilia mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi mpaka mchezaji huyo, 33, atakapoweka wazi kuwa anataka kuondoka Barcelona. (Marca-in Spanish)

Romelu Lukaku
Getty Images
Chelsea wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 86.3 kutoa Romelu Lukaku Milan

Chelsea wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 86.3 kwa ajili ya mshambuliaji Mbelgiji anayecheza katika klabu ya Inter Milan Romelu Lukaku, 27, endapo the Blues watashindwa kumsajili mshambuliaji Erling Braut Haaland,20, wa Borussia Dortmund (Calciomercato-in Italian)

Tottenham watajaribu kumsajili mlinzi wa kati wa Southampton Jannik Vestergaard,28, mwenya thamani ya pauni milioni 18, baada ya dirisha la usajili kufunguliwa. (Express)

Liverpool wameiambia RB Leipzig kuwa hawatamsajili mlinzi wa kati, Mfaransa Ibrahima Konate,21, (Bild, via Express)

Ibrahima Konate
Getty Images
Liverpool imesitisha mpango wa kumsajili mlinzi wa RB Leipzig Ibrahima Konate

Reds watakabiliwa na ushindani wa Chelsea katika kumnasa kiungo wa kati wa Ajax Ryan Gravenberch,18, ambaye anatazamwa kuwa mbadala wa Georginio Wijnaldum,30. (Gazzetta dello Sport,via Express)

Kocha wa zamani wa Bournemouth anamtaka mshambuliaji wa Everton Josh King,29, kuwa mchezaji wa kwanza kumsajili akiwa kocha wa Celtic. (Sun)

Dembele
Getty Images

Barcelona wanataka kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa Kifaransa Ousmane Dembele mpaka mwaka 2025. Klabu hiyo ya La Liga inamtaka mchezaji huyo mwenye miaka 23 ambaye mkataba huo unamalizika mwaka 2022- apatikane katika soko la usajili iwapo makubaliano hayatafikiwa. (Sport-in Spanish)

Barcelona wameendelea kumfuatilia mlinzi wa Manchester City, Mhispania Eric Garcia lakini wametoa ofa pungufu ikilinganishwa na iliyowekwa mezani mwaka jana uliopita. (Marca)

Bayern Munich imethibitisha kuwa mlinzi wa Kijerumani Jerome Boateng, 32, ataondoka kwenye klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika msimu huu. (Sky Sports, via Goal)

Bayern Munich imethibitisha kuwa mlinzi wa Kijerumani Jerome Boateng, 32, ataondoka klabu hiyo
Getty Images
Bayern Munich imethibitisha kuwa mlinzi wa Kijerumani Jerome Boateng, ataondoka klabu hiyo

Southamp na West Ham ni miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa na kiungo wa kati wa Manchester City Yangel Herrera,23, ambaye anacheza kwa mkopo katika klabu ya Granada. (Goal)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anamtaka Lucas Torreira kuwa na subira baada ya kiungo wa kati wa Uruguay,25, ambaye anacheza kwa mkopo Atletico Madrid, kuomba kuwaacha washika bunduki hao kwenda Boca Juniors. (Mirror)