Sadio Mane: Je kuondoka kwa mshambuliaji huyo wa Liverpool kuna athari gani?

21 Junio, 2022

Sadio Mane (centre)
Getty Images

Ni ishara ya mchezaji mzuri sana wakati hata shangwe za kumsajili mmoja wa washambuliaji wenye vipaji vya hali ya juu haziwezi kufidia kabisa kuondoka kwake.

Hapa ndipo mahali ambapo Liverpool wanajikuta - wakifurahishwa na ujio wa Darwin Nunez, lakini wakihuzunishwa na mwisho wa nyota ya Sadio Mane miaka sita katika uwanja wa Anfield.

Uhamisho wa Mane kwenda Bayern Munich unaacha mmoja wa washambuliaji wakubwa zaidi wa ligi ya Premier katika historia kutohusishwa na timu muhimu - ambayo amefunga mabao 120 katika mechi 269 na kuisaidia Liverpool kushinda kila taji kubwa linalopatikana.

BBC Sport inaangazia athari za mshambuliaji huyo wa Senegal katika wLiverpool na kile ambacho washambuliaji wa timu hiyo watahitaji ili kustawi bila yeye.

Amekuwa mchezaji wa haiba ya kiwango cha juu

Wakati ambapo msimu ulikuwa ukiendelea huku kukiwa na majadiliano mengi ya kuthibitisha kandarasi mpya ya mane , Mohamed Salah au Roberto Firmino zaidi yam waka 2023, uwezekano wa mmoja wao kuondoka ulizidi.

Kabla ya fainali ya kombe la klabu bingwa na Real Madrid, Salah aliahidi atakuwa katika klabu hiyo msimu ujao , lakini Mane hakutaka kuzungumzia kuhusu hatma yake.

Kuondoka kwake kunaathiri awamu ya kwanza ya uongozi wa Jurgen Klopp kama meneja, ambapo klabu hiyo imepanda hadi kileleni mwa mchezo wa kimataifa.

Mane alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na mkufunzi huyo wa Liverpool , kutoka Southampton adi Merseyside kwa dau la £34m mwaka 2016.

Mabao yake 13 katika msimu wake wa kwanza yalisaidia Liverpool kurejea Ligi ya Mabingwa baada ya misimu kadhaa nje ya michuano hiyo, na hivyo kutengeneza njia ya mafanikio ya ajabu yaliyofuata.

Ndani ya miaka miwili walikuwa mabingwa wa Ulaya na miezi 12 baadaye wakashinda Ligi Kuu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30.

Pia wamekuwa washindi wa pili wa Ligi ya Mabingwa mara mbili na kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu mara mbili, ikiwemo msimu wa 2021-22 ambao walishinda kombe la FA na Kombe la Ligi.

The summer after Mane's arrival, Salah signed and, along with Firmino, formed one of the finest forward lines in English football history. It produced 338 goals in five seasons in all competitions.

Baada ya kuwasili kwa Mane, Salah alisajiliwa pamoja na Firmino, na wakaunda safu ya bora zaidi ya mashambulizi katika historia ya soka ya Uingereza. Safu hiyo Ilizalisha mabao 338 katika misimu mitano katika mashindano yote.

Sadio Mane's six seasons at Liverpool
BBC Sport

Kwa wakati huo, Mane ameonyesha uwezo wa kutosha wachache wanaweza kumiliki , akicheza upande wa kulia katika msimu wake wa kwanza, kisha kubadili nafasi ya upande wa kushoto ili kushirikiana na Salah na, hivi majuzi, akicheza katikati.

Huku watatu hawa wakiingia au kukaribia miaka ya 30, mabadiliko ya safu ya mashambulizi ya Liverpool yalikuwa tayari yanaendelea kabla ya kuondoka kwa Mane, kwa kusajiliwa na kuunganishwa kwa Diogo Jota na Luis Diaz na ununuzi wa hivi majuzi wa vijana wenye vipaji vya kusisimua Fabio Carvalho kutoka Fulham.

Kusajiliwa kwa Nunez kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi kufunguliwa ilikuwa ni uhamisho mwingine wa makini kutoka kwa Liverpool.

Mane, hata hivyo, hajaonyesha dalili zozote za kufifia. Mbali na hilo. Kiwango chake katika kipindi cha pili cha 2021-22 kilikuwa cha kipekee, na kuchangia kama mtu yeyote katika kilabu hiyo.

Alifunga nyumbani na ugenini dhidi ya Villarreal katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. Ni bao lake lililoiwezesha Liverpool kupata pointi kwenye Ligi ya Premia dhidi ya Manchester City mwezi Aprili na bao lake la kichwa ambalo liliweka hai jitihada zao za kutwaa ubingwa dhidi ya Aston Villa mwezi uliofuata.

Kwa jumla alitikisa nyavu mara 13 katika michezo 27 - akicheza kwa kiasi kubwa kama nambari tisa - baada ya kusaidia Senegal kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika mnamo Februari. Alifunga penalti ya ushindi kwenye mikwaju ya penalti dhidi ya Misri kwenye fainali.

"Kwa miaka minne au mitano iliyopita amekuwa mtu asiyebashirika," kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City na kiungo wa kati wa Ivory Coast Yaya Toure aliiambia BBC World Service.

"Without any disrespect to Mohamed Salah, who was done brilliantly as well, Raheem Sterling, Lionel "Bila ya kumdharau Mohamed Salah, ambaye amefanya kazi nzuri, Raheem Sterling, Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, unawezaje kuniambia kijana huyu hayupo kwenye wachezaji watatu bora wa Ballon d'Or? Inawezekanaje?

"Katika muda wote wa kushinda mataji, yuko juu. Liverpool kwa sasa wako kila mahali - Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Premia, Kombe la FA, Kombe la Ligi."

Huku Mane sasa akijiunga na Divock Origi katika kuondoka katika uwanja wa Anfield na Takumi Minamino pia akiondoka, macho yote yataelekezwa kwa mchezaji atakayekuja kuimarisha safu ya mashambulizi ya Liverpool.

Nadharia ya mabadiliko ya Darwin

Uwezo wa kufunga magoli ndio kipaji kikuu cha Sadio mane huku huku mshambuliaji huyo akiwa na wastani wa mabao 20 kwa msimu katika michuano yote huko Liverpool, mengi yakiwa yamepangwa vizuri na mengine ya kunyang'anya kwa mara ya kwanza kwa kutumia miguu au kichwa.

Mane ana ufahamu mkubwa na wakati wa kupata nafasi na kuitumia vyema. Kinachohusishwa na hili ni uwezo wake wa kupiga chenga na kupiga pasi, hivyo kumfanya awe adui mgumu nje ya eneo la hatari.

Nguvu na kasi ni rasilimali kubwa kwake, sio tu katika kusaidia uwezo wake wa ushambuliaji, lakini kwa kile anacholeta kwa timu inayopenda kuzuia kwa ukali kutoka mbele.

Kulingana na tovuti ya takwimu za kandanda FBref.com, mbinu makini ya Liverpool kwenye soko tayari imeshazaa matunda, huku Diaz na Jota wakimkaribia Mane kwa ujuzi katika safu ya winga na washambuliaji mtawalia.

Jota alifanikiwa kuzalisha magoli kama ya Mane 21 na kusaidia mara nane , na hivyobasi kusaidia katika mchezo wa kuwasukuma nyuma wapinzani na kuonesha uwezo wa kutamba katika safu ya mashambulizi.

Katika miezi michache, Diaz ameonesha kwamba anaweza kutoa usaidizi wa magoli, mengi kutoka upande wa kushoto wa mashambulizi kutokana na uwezo wake wa kuweza kutamba na boli mbele ya adui na kusababisha magoli mengi

Msimu uliopita mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alifunga mabao 34 katika mechi 41 alizochezea Benfica, yakiwemo magoli mawili dhidi ya Liverpool katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa. Lakini kutokana na mchezo mzuri wa kipwa wa Liverpool Alisson, angeweza kuwa na matatu au manne katika uwanja wa Anfield pekee.

Akiwa na kasi, ustadi, na mshikaji mpira mahiri - ni wazi kuona kwa nini Klopp anafurahia sana usajili wa Nunez, akiambia tovuti ya Liverpool: "Ana kila kitu tunachohitaji. Anaweza kuweka tempo, kuleta nguvu, anaweza kusababish hatari kutoka nafasi ya kati na wingi na yeye ni hatari na mwenye nguvu katika hatua zake."

Kama Klopp pia alivyotambua, raia huyo wa Uruguay ni "kazi inayoendelea" ambaye atapewa muda wa kujiendeleza kama sehemu ya "chaguo zuri la mashambulizi''

Mane anaweza kuwa alishinikiza kuondoka kwake, lakini katika upangaji wao wa ustadi wa siku za mbele na kutumia pesa nyingi kupata talanta ya hali ya juu, Liverpool wamejaribu kupunguza kipindi cha mpito kwa kile ambacho kinaweza kuwa safu nyingine ya tatu inayoogopwa kote duniani.