Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 07.06.2022. : Salah, Bale, Mane, Bergwijn, De Ligt

07 Junio, 2022

Mshamnbuliaji wa Misri Mohamed Salah
BBC
Mshamnbuliaji wa Misri Mohamed Salah

Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 29, amewaambia marafiki wake wa karibu kwamba alikuwa tayari kujitolea kuichezea klabu yake ya Liverpool kwa siku zijazo lakini aliamua kurejea tena Barcelona baada ya kumuahidi kuhamia katika Nou Camp msimu ujao. (Mirror)

Tottenham hawana mipango ya kusaini mkataba na nahodha wa Wales Gareth Bale kwa mara ya tatu kwani winga huyo mwenye umri wa miaka 32 bado anatafakari kuhusu ni wapoi atakapojiandaa kwa ajili ya Kombe la Dunia la mwaka huu. (Telegraph)

Sadio
Getty Images
Mshambuliaji Msenegal Sadio Mane

Mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 30, tayari amekwishamuomba mchezaji mwenzake katika timu ya Liverpool kiungo wa zamani wa Bayern Munich Thiago Alcantara iwapo anaweza kuhamia katika nyumba yake katika Munich iwapo atajiunga na Machampioni wa Bundesliga msimu huu. (Mail)

Barcelona wako tayari kwa mazungumzo na Manchester United kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Mholanzi Frenkie de Jong, 25, kuelekea Old Trafford lakini klabu hiyo ya Uhispania bado haijapokea ofa rasmi kutoka United. (Sport - in Spanish)

Meneja Mholanzi Louis van Gaal
Getty Images
Meneja Mholanzi Louis van Gaal

Meneja Mholanzi Louis van Gaal anasema mshambuliaji Mholanzi Steven Bergwijn, 24, anahitaji kuondoka Tottenham na kujiunga na Ajax " haraka iwezekanavyo." (De Telegraaf via Evening Standard)

Spurs wanataka malipo ya Euro milioni 30 (£25.6m) ili kumuacha Bergwijn ajiunge na klabu nyingine msimu huu. Mchezaji huyo pia analengwa na mahasimu wao katika Primia Ligi -Everton, huku Mchampioni wa Uholanzi wakiwa bado wanashugulikia dau lake (Fabrizio Romano)

G
Getty Images
Chelsea wana nia na mlizi wa Juventus Mholanzi Matthijs de Ligt

Chelsea wana nia na mlizi wa Juventus Mholanzi Matthijs de Ligt, 22, lakini mchezaji anayelengwa zaidi na meneja wa Blues Thomas katika safu ya ulinzi bado na kiungo kiungo wa kati-nyuma Mfaransa Jules Kounde. (talkSPORT)

Mkurugenzi wa mchezo wa Newcastle Dan Ashworth ameripotiwa kupatia kipaumbele mpango wa kumleta winga mpya wa kulia msimu huu, huku Bayer Mchezaji wa kimataifa wa Leverkusen na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Moussa Diaby, 22, na mshambuliaji wa Watford na Senegal Ismaila Sarr, 24, wakiwa kwenye orodha. (Sky Sports)

Mholanzi anayecheza nyuma-kulia -Denzel Dumfrie
Getty Images
Mholanzi anayecheza nyuma-kulia -Denzel Dumfrie

Manchester United na Bayern Munich wako makini katika kusaini mkataba na mchezaji mwenye kiwango cha juu katika Inter Milan Mholanzi anayecheza nyuma-kulia -Denzel Dumfries, 26, msimu huu. (Calciomercato via Mail)

Mlinzi Mholanzi Sven Botman, 22, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Newcastle, anasema kuwaAC Milan bado wanaufanyia kazi mkataba kukamilisha kusainiwa kwa mkataba wake utakaomuondoa katika klabu Lille. (Football Italia)

Kiungo wa safu ya kati-nyuma Muingereza James Tomkins, 33, ameripotiwa kusaini mkataba mpya na Crystal Palace, huku kiungo wa kati Mskochi James McArthur, 34, akiaminiwa kukubali mkataba mpya katika klabu hiyo ya Selhurst Park. (Sun)